NASA kugharamikia mazishi ya waliouliwa

NASA kugharamikia mazishi ya waliouliwa

Mike Nyagwoka

Kinara wa NASA, Raila Odinga amehudhuria shughuli ya kuondoa mili ya watu waliouliwa wakati wa makabiliano na polisi, katika Hifadhi ya Maiti ya City, jijini Nairobi. Takriban mili 10  ya watu hao ambao vifo vyao vinasemakana kutokana na dhuluma za polisi inatarajiwa kusafirishwa leo kuelekea maeneo mbalimbali nchini kwa mazishi. Kufikia sasa mili iliyoondolewa ni ya, George Owino, Kennedy Owino, Mary Atieno, Evans Owino, Elvis Otieno, Omondi Ojwanga na Geoffrey Mutinda.

Muungano wa NASA umeahidi kugharimia mazishi hayo. Kwa mujibu wa Raila, watu 215 waliuliwa na polisi katika kipindi cha uchaguzi kuanzia mwezi Agosti na kuitaka serikali izifidie familia zilizoathirika. Licha ya vifo hivyo kuhusishwa na polisi, idara hiyo wamekana kuhusika na kusema baadhi yao waliuliwa na umati walipokuwa wakitekeleza uhalifu.