NASA YAIPA MATAKWA IEBC

NASA YAIPA MATAKWA IEBC
BY Rosa Agutu
Kuhusu matakwa yaliyotolewa na NASA kabla ya kushiriki uchaguzi ni kwamba matokeo ya urais yatangazwe katika maeneo bunge na kabla matokeo kupeperushwa katika kituo cha kitaifa cha kuhesabia kura. Aidha wanasema ni lazima maajenti wa vyama wapewe fursa ya kuidhimnisha matokeo na kukagua mashine ya kupeperusha matokeo.
Wanasema ni sharti Form 34B zote zichapishwe upya zikiwa na majina ya vituo vya kupigia kura na wagombea. Vilevile maafisa wa kusimamia uchaguzi wa maeneo bunge wanastahili kujaza fomu hizo kwa kalamu kabla ya kutangazwa. NASA inasema hakuna matokeo yatapeperushwa kupitia ujumbe mfupi. Mpangilio huo utashuhudiwa na maajenti wa vyama, vyombo vya habari, waangalizi na umma.
Vilevile imetangaza kuwa uchunguzi wao umeonesha kwamba form 34B themanini hazikuwa halali, hivyo kutaka maafisa wa IEBC walioruhusu fomu hizo kutumika kufutwa kazi. Maafisa hao ni Ezra Chiloba, Abdi Guliye, Marijan Hussein Marijan, Betty Nyabuto, James Muhati, Immaculate Kassait, Praxedes Tororey, Moses Kipyegon, Sidney Namulungu, Nacy Kariuki na Silas rotich.
Aidha, viongozi wa NASA wanataka kwamba kabla ya kura kuanza kuhesabiwa saa kumi na moja jioni ni lazima idadi kamili ya walio-piga kura itangazwe kulingana na mashine ya KIEMS.
NASA aidha inataka waatalamu wa kimataifa wasimamie uchaguzi huo huku wakisaidiwa na Tume ya IEBC pamoja na maagenti wa vyama. Muungano huo umesema Jumapili ijayo utaandaa mkutano mkubwa wa kisiasa katika Uwanja wa Jacaranda jijini Nairobi.