MIILI YA WATOTO WA MGOMBEA MWAKILISHI WADI RATEMO YAPATIKANA

MIILI YA WATOTO WA MGOMBEA MWAKILISHI WADI RATEMO YAPATIKANA

Na Sophia Chinyezi

Wingu la simanzi lingali limetanda katika mtaa wa Kapsoya mjini Eldoret baada ya miili ya watoto watatu wa mgombea wa wadhifa wa Uwakilishi Wadi James Ratemo kupatikana katika mto Nzoia. Watoto wao walitoweka siku ya Jumamosi walipokuwa wamekwenda kuhudhuria ibada katika kanisa la Eldovi SDA.
Mjomba wa watoto hao, Peter Lukoye amethibitisha kupatikana kwa mili ya watoto hao Clifford Nyambane, Dan Nyamweya na Glen Ongagi. Familia hiyo imewalaumu maafisa wa usalama wa eneo hilo kwa madai ya kutochukulia taarifa ya kutoweka kwa watoto hao kwa uzito, licha ya ndugu ya baba ya watoto hao Enoch Onsanze kukamatwa kwa kushukiwa kuwa mshukiwa mkuu, kwani yeye ndiye aliyekuwa nao wa mwisho.
<AUDIO> 8035
Ratemo anawania wadhifa huo kwa tiketi ya chama cha KANU na kufikia sasa, haijabainika iwapo kisa hicho kina uhusiano wowote na azma yake ya kisiasa.