Peter Kenneth kuania ugavana kama mgombea huru

Peter Kenneth kuania ugavana kama mgombea huru

Na Rose Agutu
Mwanasiasa Peter Kenneth amesema Gavana Kidero amefeli katika utendakazi wake, huku akisistiza kwmaba Seneta Mike Sonko vilevile amechangia kutoendelea kwa kaunti hii. Akizungumza na wanahabari wakati wa kutangaza kujiuzulu kuwa mwanachama wa Jubilee, Kenneth amesema atawania wadhifa wa Ugavana Nairobi akiwa mgombea huru.

Aidha, Kenneth amesikitishwa na jinsi uteuzi wa chama hicho ulivyoendeshwa jijini Nairibi, na kusisistiza kwamba kulikuwapo na wizi wa kura. Aidha ameeleza imani kwamba ataibuka mshindi wakati wa uchaguzi mkuu wa Agosti 8.

Ikumbukwe Kenneth alishindwa na Mike Mbuzi Sonko katika uteuzi wa Chama cha Jubilee baada ya Sonko kupata kura elfu mia moja thelathini na nane, mia moja themanini na tano huku Kenneth akipata kura elfu sitini na mbili, mia tano na nne.