Eneo la Kati laelekea kuvunja daraja la BBI badala ya kulijenga

Naibu Rais William Ruto na Kasisi Peter Kania, katibu wa PCEA, kwenye hafla ya kuadhimisha miaka 50 ya kanisa hilo eneo. [Picha, Standard]

Hata kabla ya ripoti kamili kutolewa, tayari Rais Uhuru na kiongozi wa upinzani Raila Odinga wamewadhihirishia wakenya kwamba wako tayari kufa kupona kutetea mpango wa kujenga madaraja ya uhusiano mwema maarufu Building Bridges initiative – BBI.

Uhuru na Raila wameapa kuzunguka nchi nzima kueneza ujumbe wa kuwarai wananchi kuunga mkono mapendekezo ya ripoti ya BBI wakidai kwamba BBI ndio njia ya pekee ya kusuluhisha matatizo yaliyoandama nchi tangu jadi.

Idadi kubwa ya viongozi miongoni mwao wandani wa Rais Uhuru Kenyatta kutoka mkoa wa kati tangu enzi za KANU wameonyesha dalili za kupinga ripoti ya BBI wakisema hawatounga mkono mageuzi ya kikatiba yatakayohujumu eneo wanaloliwakilisha. 

Zaidi ya wabunge wapatao 40 kutoka Baraza la Seneti na Bunge la Taifa kutoka eneo la Mkoa wa Kati wanaiunga mkono ripoti hiyo.

Mgao mdogo wa fedha kutoka kwa serikali ya kitaifa kwa eneo hilo ilihali ni eneo lenye idadi kubwa ya watu ndio sababu kubwa ya wabunge hao kutoa ilani ya mapema ya kutounga mkono ripoti ya BBI.

Viongozi hao aidha wanasema kwamba ikiwa matakwa yao hayatohusishwa kwenye mapendekezo Kundi hilo la viongozi kutoka eneo la kati mwa nchi lilimjumuisha waziri wa kilimo Mwangi Kiunjuri. Kwa mda wa hivi karibuni Rais Uhuru Kenyatta ameonekana kupata upinzani mkali sana kutoka kwa baadhi ya viongozi kutoka eneo lake la kati.

Mnamo mwezi Juni mwaka huu ya ripoti ya BBI hawatakuwa na la ziada ila kuipinga. 

Wabunge hao ni kutoka Kaunti za Nakuru, Laikipia, Embu, Tharaka Nithi na Meru.

Msemaji wao ambaye ni seneta wa Meru Mithika Linturi alidokeza kwamba msimamo huo unaungwa mkono na viongozi wengine wengi kutoka eneo hilo alipohudhuria kongamano la kitaifa la dhehebu la Akorino Rais alionyesha kugadhabishwa na hatua ya baadhi ya viongozi wanaonekana kuvuta upande wa pili na kutatiza ajenda yake ya maendeleo akiwaita wakora huku akiwaonya kuwa yeye si mdogo wao.

Yamkini miezi mitano baadaye onyo kali linajidhihirisha kutoka kwa eneo lilo hilo ingawa Rais hajaonekana kufanya mikutano ya hadhara kama njia ya kuwanyamazisha wapinzani wake kutoka eneo la mkoa wa kati hivi karibu.

Ripoti ya BBI ilinatarijiwa kuwasilishwa kwake baada ya jopo hilo kutangaza kwamba wanasubiri tu siku rasmi ya kuiwasilisha kwa Rais.

Wiki mbili zilizopita Rais Uhuru aliapa kuwa atazunguka kote nchini kuwarai wakenya kuunga mkono mapendekezo ya ripoti hiyo, “tutarejea hivi karibu na ripoti ya BBI na msije mkahadaiwa na yeyote kuwa ni siasa tutakuwa tunafanya,” alisema Rais.  

“kama kuna urithi namuomba mungu anisaidie kuufanikisha kwa niaba ya wakenya wengi kwani hatustahili tena kumwaga damu kwa sababu ya mizozo ya matokeo ya uchaguzi,” alisema Rais wakati wa kuzindua mkondo wa Reli ya kisasa ya Nairobi kwenda Naivasha.

Hata hivyo wabunge wa eneo la kati mwa Kenya wanasema punde tu ripoti itakapotolewa watakongamana ili kutoa msimamo mmoja kuhusu mapendekezo ya ripoti ya jopo hilo la BBI lililobuniwa baada ya Uhuru na Raila kukubali kufanya kazi pamoja.  

Viongozi hao wanaonya kwamba wataipinga ripoti hiyo ikiwa haitotatua swala la uwakilishi na rasilmali zinazotengewa eneo la Mkoa wa Kati.