Ningehudhuria mazishi ya Kibaki, moyo wangu ungetulia-Allan Makana ''Mjukuu wa mbali wa Kibaki''

General Podcasts | 1 week ago

Allan Makana maarufu Mjukuu wa Kibaki asiye wa karibu anasema alifutwa kazi baada ya kuzua sarakasi katika hafla ya kuutazama mwili wa Kibaki. Anasema alifanya hivyo kwa sababu anaamini ni mjukuu wa Kibaki. Lakini vipi? Kulingana naye, alimpa Kibaki heshima kwa kujitambulisha kuwa mjukuu wake kutokana na kuanzisha mfumo wa masomo bila malipo uliomfaidi pakubwa. Makana anasimulia chimbuko la haya yote katika Podcast yetu akizungumza na mwanahabari wetu Esther Kirong'