SECTIONS
Premium

Nduguye Naibu wa Rais, Rigathi Gachagua, Jack Reriani ameaga dunia

Ndugu wa Naibu wa Rais, Rigathi Gachagua, Jack Reraini amefariki dunia.

Kupitia mtandao wa Twitter, Rigathi amemwomboleza nduguye mkubwa aliyefariki dunia jana usiku. 

Naibu wa rais amesema kifo cha nduguye kimemvunja moyo, na kwamba sasa amesalia kuwa mwana wa pekee katika familia kufuatia vifo vya ndugu zake.

Viongozi mbalimbali akiwamo Mama wa Taifa Rachel Ruto, Spika wa Bunge la seneti Amason kingi ni miongoni mwa waliotuma risala za rambirambi kwa familia ya Rigathi wakati huu msiba.