DIDA AKOSOA MAANDAMANO YA NASA

DIDA AKOSOA MAANDAMANO YA NASA
Rosa Agutu

Kiongozi wa Chama cha Alliance for Real Change, Abduba Dida amekosoa maandamanao yanayoandaliwa na Muungano wa NASA hapo kesho ya kutaka kuondolewa kwa maafisa kadhaa wa Tume ya IEBC kabla marudio ya uchaguzi wa urais Oktoba 26 na kumtaka Kinara wa Muungano huo, Raila Odinga kufuata sheria bila kutumia maandamano.
Akiwahutubia wanahabari jijini Nairobi, Dida ameitaka mahakama kueleza ni kwa nini wagombea wawili ndio watakaoshiriki uchaguzi huo ilhali kulingana na sheria, ilhali ni marudio ya kura ya urais wala si duru ya pili ya uchaguzi.
Dida vilevile amesema maafisa wa IEBC waliotajwa na NASA wanastahili kujiuzulu na kudai kwamba Mwenyekiti wa tume hiyo, Wafula Chebukati hatumii mamlaka aliyo nayo kisheria kutekeleza mabadiliko.

Related Topics