Washiriki 44 wajiandikisha kushiriki maonyesho ya magari yanayodhaminiwa na benki ya CBA

Sports | Monday 20 Mar 2017 9:22 pm

Washiriki 44 wamejiandikisha kushiriki maonyesho ya magari yanayodhaminiwa na benki ya CBA ya Concours d’Elegance. Hadi sasa kuna idadi ya magari 23 na pikipiki 21 huku 12 zikiwa zimetoka nchini Uganda. Awamu ya mwaka huu itakuwa ni ya sita kudhaminiwa na benki ya Commercial Bank of Africa na ya  47 kudhaminiwa na klabu ya wamiliki wa Alfa Romeo. Maonyesho haya yatafanyika mwezi wa  Septemba tarehe 24 katika uwanja wa mashindano haya wa Nairobi Racecourse.