Polisi huko Nyandarua waanzisha uchunguzi kwa chifu anayedaiwa kuhusiana na kunajisi watoto

KTN Leo | Monday 20 Mar 2017 8:59 pm

Polisi huko Nyandarua wameanzisha uchunguzi kuhusu madai kwamba chifu, naibu wake na baadhi ya walimu wamekuwa wakishirikiana katika kuwanajisi wasichana wadogo, mbali na kuwadhulumu wanawake kimapenzi. Mapema leo wakazi wa kijiji cha Rutara, eneo la Mirangire, waliandamana  kulaani matendo ya naibu mmoja wa chifu anayedaiwa kumnajisi msichana mmoja yatima mwenye umri wa miaka kumi na minne, aliyekuwa amekwenda ofisini mwake kutafuta msaada.