Seneta Mike Mbuvi Sonko awasilisha stakabadhi kwa chama cha Jubilee

Dira ya Wiki | Friday 17 Mar 2017 8:51 pm

Shughuli ya kuwasilisha stakabadhi za uteuzi katika chama cha Jubilee imekamilika leo na kufungwa na mgombea wa kiti cha ugavana katika kaunti ya Nairobi Mike Mbuvi Sonko. Sonko aliwasili katika makao makuu ya chama hicho akiwa ameandamana na wafuasi kiasi cha haja, na viongozi wengine katika kundi la ‘team Nairobi’ wakiwemo wagombeaji wa nafasi tofauti. Sonko amesisitiza kuwa ulikuwepo mpango wa kumfungia nje ya kinyanganyiro cha kuwania kiti cha ugavana ila katika dakika za lala salama akafanikiwa kupata stakabadhi muhimu zilizokuwa zinamzuia kufika mbele ya kamati ya uchaguzi ya chama cha Jubilee.