KANU yawapokea wagombezi 48 kutoka maeneo ya Isiolo, Marsabit na mlima Elgon

Dira ya Wiki | Friday 17 Mar 2017 8:47 pm

Chama cha KANU leo hii kimepokea wagombezi 48 kutoka maeneo ya Isiolo, Marsabit na mlima Elgon. Akizungumza wakati wa kupokea wagombezi hao wa usenata, ugavana na ubunge, katibu mkuu wa chama hicho amesisistiza msimamo wao wa kumuunga mkono rais Uhuru Kenyatta kwenye uchaguzi ujao huku akitaja imani yao kwamba wagombezi hao wataibuka washindi.