Wavuvi watano wamefariki baada ya boti lao kuzama ziwa Victoria huko Budalang’i-Busia

Dira ya Wiki | Friday 17 Mar 2017 8:46 pm

Wavuvi watano wamefariki baada ya boti lao kuzama ziwa Victoria huko Budalang’i kaunti ya Busia. Boti hilo ambalo linadaiwa kuwabeba watu zaidi ya inavyostahili ilikuwa na abiria 18 ambao ni wavuvi waliokuwa wakisafiri kutoka nandekhe hadi runyu. Miili mitatu imeopolewa huku shughuli za kutafuta mingine miwili ikiendelea.  Wapiga mbizi wanaendeleza shughuli hiyo.