IEBC yaanza rasmi mchakato wa usajili wapiga kura raia wa Kenya wanaoishi Tanzania

KTN Leo | Wednesday 22 Feb 2017 7:54 pm

Tume huru ya uchaguzi IEBC leo ilianza rasmi mchakato wa usajili wapiga kura raia wa Kenya wanaoishi Tanzania hasa katika miji ya Arusha na Dar es Salaam.  Japo mchakato huo umechelewa na ilipangwa kuanza tarehe 20 ya mwezi huu lakini wakenya waishio nchini Tanzania katika jiji la Dar es Salaam wamepongeza hatua ya tume ya uchaguzi kuwasogezea kituo cha kujisajili  hivyo watakuwa na haki ya kupiga kura katika uchaguzi mkuu ujao.