James Onyango ambwaga Patrick Atuharwe kwenye ndondi katika kitengo cha welterweight

KTN Leo | Sunday 19 Feb 2017 7:50 pm

Bingwa wa ndondi katika kitengo cha welterweight kwenye mashindano ya  jumuia ya madola James Onyango aliibuka na ushindi kwenye pigano lake hapo jana usiku dhidi ya Patrick Atuharwe kutoka Uganda . Onyango alimbwaga mwenzake katika raundi ya pili ya pigano hilo ambalo liliandaliwa mjini Nairobi. Kwenye pigano jingine , bingwa wa uzani wa juu humu nchini Maurice Okolo alitikisa upinzani mkali kutoka kwa mwanabondia wa Malawi Alick Gogodo  na kumbwaga chini. Bingwa wa dunia katika uzani wa Super Bantam Weight  Fatuma Zarika aliwatumbuiza mashabiki waliokuwa wamejaa kwenye ukumbi huo akimwangusha Flora Machela kutoka Tanzania katika pigano lilochukua muda wa chini ya dakika mbili.