KTN Leo: Hazel Katana ajiunga na Jubilee akisema amechoshwa na ODM

KTN Leo | Saturday 28 Jan 2017 7:50 pm

Katika kile kinachoonekana kuwa kuchacha kwa siasa za Pwani naibu Gavana kaunti ya Mombasa Hazel Katana amekihama chama cha ODM na kujiunga na chama cha Jubilee. Amesema atawania useneta wa Mombasa wakati wa uchaguzi mkuu ujao. Je hatua hiyo ina maana gani kisiasa kwa misingi kuwa Gavana Ali Hassan Joho amekuwa na ufuasi mkubwa Mombasa?