KTN Leo: Aliyekuwa mbunge wa Garsen, Darson Mungatana ajitenga na madai ya ubadhirifu wa milioni 51

KTN Leo | Monday 16 Jan 2017 7:32 pm

Aliyekuwa mbunge wa eneo Garsen ambaye pia anawania kiti cha ugavana kaunti ya Tana river Danson Mungatana, amejitenga na madai ya kuhusika katika ubadhirifu wa takriban shilingi milioni 51 kaunti ya Kilifi. Akiwahutubia wanahabari kaunti ya Nairobi, Mungatana amedai, nia ya gavana wa Kilifi Jeffery Amason Kingi kumhusisha na suala hili ni kumchafulia jina ili kumharibia nia yake ya kuwania kiti cha ugavana. Amedai kwamba hajawahi kufanya biashara na serikali ya kaunti ya Kilifi wala kumiliki kampuni zilizotajwa.