Kijana aliyepita mtihani wake wa KCPE apata usaidizi wa kuendeleza masomo ya shule ya msingi

KTN Leo | Wednesday 11 Jan 2017 7:39 pm

Mwanafunzi mmoja kutoka familia  isiyojiweza lakini aliyefanya vyema katika mtihani wa KCPE na kuibuka katika nafasi ya kwanza alikosomea, amepata msisimko wa aina yake. Baada ya kisa chake kuangaziwa na gazeti la The Standard, muungano wa marubani wastaafu katika jeshi la angani nchini waliguswa na kisa cha mvulana huyo na kumsaidia. kijana Muriuki Nderitu aliyepata alama 372 amekuwa akifanya kazi katika matimbo ya chaka kieni ili kujaribu kutafuta pesa za karo ili ajiunge na shule ya sekondari ya Nyeri High. Marubani hao wastaafu, walifika kwa ndege  na kumchukua  kijana huyo kutoka shule ya msingi ya Karicheni alikomaliza hadi shule ya sekondari ya Nyeri High. Tayari wamemlipia karo yote ya kidato cha kwanza na baada ya hapo wataendelea kumlipia karo hadi atakapomaliza kidato cha nne.