KTN LEO: Jamii ya Wahindi wanaoishi Kenya wataka kutambuliwa kama kabila mojawapo nchini

KTN Leo | Wednesday 11 Jan 2017 7:33 pm

Jamii ya Wahindi wanaoishi humu nchini sasa wanataka kutambuliwa rasmi kama kabila la arobaini na nne. Wakizungumza na wanahabari katika hoteli moja hapa jijini, jamii hio waliotokea bara la Asia, wamesema tayari wameuasilisha mswada rasmi kwa Rais Uhuru Kenyatta, wakimtaka aanzishe mchakato wa kisheria ili kuwatambua rasmi kama mojawapo ya makabila yaliyomo humu nchini.