Mbiu ya KTN: Mfanyabishara mmoja akadiria hasara ya mamilioni huko Migori

KTN Mbiu | Wednesday 11 Jan 2017 6:33 pm

Mfanyibiashara mmoja viungani mwa mji wa Migori anaendelea kukadiria hasara ya milioni ya pesa baada ya moto kuteketeza duka la kuoka mikate katika eneo la Nyasare kwenye kaunti ya Migori. kulingana na walioshuhudia kuanza kwa moto huo duka la kuoka mikate la mfanyibiashara huyo Ahmed Jamal Salah liliteketea kwa muda wa saa moja kabla ya gari la zima moto la kampuni ya sukari ya Sony kufika. Jumba hilo  la orofa tano katika barabara kuu ya Migori kuelekea Kisii likiwa tayari limeteketea.moto huo unakisiwa kusababishwa na hitilafi za nguvu za umeme