KTN Leo: Awamu ya kwanza ya mahojiano na makamishina wa IEBC imefanyika leo

KTN Leo | Tuesday 10 Jan 2017 9:39 pm

Awamu ya kwanza ya mahojiano ya orodha iliopendekezwa na Rais kwenye nyadhifa za tume ya uchaguzi, IEBC, imefanyika leo.  Aliyependekezwa kwenye nafasi ya mwenyekiti Wafula Chebukati alijitetea kuhusiana na kufaa kwake kwenye nafasi hiyo huku wanaopendekezwa kwenye nafasi za  Kamishna Consolata Nkatha na wenzake wawili pia  wakikabiliana na maswali yenye uzani wa juu mbele ya kamati la Bunge kuhusu sheria.