Maandalizi ya kusajili wapiga kura yaanza Taita Taveta

KTN Mbiu | Tuesday 10 Jan 2017 6:45 pm

Huku Tume ya Uchaguzi na Mipaka nchini IEBC ikilenga kuwasajili wakenya zaidi ya milioni 6 kwenye zoezi la usajili linalotazamiwa kuanza wiki ijayo ya tarehe 16 mwezi huu, harakati za maandalizi ya shughuli hiyo zimeanza sehemu mbalimbali za Kenya huku viongozi wa siasa na maafisa wakuu wa IEBC wakiwashawishi wakenya kujitokeza. Katika kaunti ya Taita Taveta, wenyeji wametakiwa kujitokeza kwa wingi na kupata fursa ya kujiamulia mabadiliko wanayotaka.