Shule zafungwa kutokana na ukosefu wa usalama mpaka wa Kitui na Tana River

KTN Mbiu | Tuesday 10 Jan 2017 6:38 pm

Shule kadhaa katika mpaka wa Kaunti za Kitui na Tana River zimefungwa kufuatia ukosefu wa usalama.  Inaripotiwa kuwa kufikia sasa watu watatu wameuawa na wahalifu wanaoshukiwa kutoka jamii ya wasomali. Kutokana na visa vya mauaji watu wengi wamelazimika kukimbilia msituni kutafuta hifadhi ya usalama wao. Masomo ya wanafunzi pia yamevurugwa na sasa hali hiyo inaimulika idara ya usalama wa ndani, wenyeji wakisubiri kuona hatua itakayochukuliwa na serikali.