Katibu mkuu wa vyama vya wafanyikazi-Francis Atwoli akashifu serikali kuwapokonya wanasiasa ulinzi

KTN Leo | Monday 9 Jan 2017 7:42 pm

Katibu mkuu wa vyama vya wafanyikazi nchini Francis Atwoli ameitahadharisha serikali dhidi ya kuwapokonya ulinzi wanasiasa wanaodhaniwa kuwa wanatofautiana na serikali kupitia kwa sera. Akizungumzia hatua ya serikali kuwaondoa walinzi wa magavana Ali Hassan Joho na Amason Kingi, Atwoli ameikosoa serikali kwa hatua hio.