Ukame unatishia maisha ya mifugo huko Tanariver

KTN Leo | Sunday 8 Jan 2017 7:29 pm

Shirika la Kenya Redcross limeanza mpango wa kuwanunua mifugo kutoka kwa jamii za wafugaji wa eneo la Tanariver  kufuatia ukame unaoyatishia maisha ya mifugo hao. Maafisa hao wanawanunua  mifugo ili kuwapa wenyeji hela za  kujikimu kimaisha wakti ambapo  baa la njaa  limeathiri maeneo mengi katika sehemu ya kaskazini mwa Pwani ya Kenya.