KTN Leo: mhariri wa KTN News-Aaron Ochieng’ afikishwa kotini akikabiliwa na kosa la wizi wa gari

KTN Leo | Tuesday 3 Jan 2017 7:32 pm

Tukienda mahakamani ni kwamba mwanahabari Aaron Ochieng’ ambaye amekuwa akifanya kazi kama mhariri hapa KTN News alifikishwa katika mahakama ya Milimani hapa Nairobi akikabiliwa na kosa la wizi wa gari.   Kiongozi wa mashtaka aliiambia mahakama kwamba mnamo tarehe 23 Disemba mwaka uliopita, Aaron kwa kushirikiana na washukiwa wengine ambao hawakuwa mahakamani, aliiba gari aina ya Mercedes Benz gari la mfanyikazi mwenzake Joy Doreen Biira.  Alikanusha  shitaka dhidi yake na kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi milioni moja au pesa taslimu shilingi laki tatu. Kesi hiyo itatajwa tena Januari 17, mwaka huu na kusikilizwa tarehe 3 februari mwaka huu.