KTN Leo Wikendi: Jamii ya Waluhya yamchangua Wycliffe Musalia Mudavadi kama kiongozi wao

KTN Leo | Saturday 31 Dec 2016 7:41 pm

Wycliffe Musalia Mudavadi ndiye msemaji wa jamii ya Abaluhyia. Hii ni baada ya kutangazwa kuwa mjumbe anayeenziwa zaidi na jamii hiyo kulinagana na utafiti uliofanywa na chuo kikuu cha Nairobi kati ya mwezi julai na oktoba mwaka huu. Waliomfuata unyo unyo ni magavana wa Kakamega Wycliffe Oparanya katika asimilia 31 sambamba na  seneta  wa Bungoma Moses Masika Wetangula. Mudavadi alipata asilimia 39 katika utafiti huo. Hebusasa tujiunge na mwanahabari Duncan Khaemba aliyeko  katika kaunti ya Kakamega ambako muda mfupi uliopita Mudavadi aliapishwa ili atupe hali ilivyo.