Mkurugenzi wa mashtaka Keriako atoa agizo la kufunguliwa mashtaka maafisa saba wa Benki ya Family

KTN Leo | Thursday 24 Nov 2016 7:38 pm

Mkurugenzi wa mashtaka Keriako Tobiko hii leo ametoa agizo la kufunguliwa mashtaka kwa maafisa 7 wa Benki ya Family kuhusiana na sakata ya Shilingi Milioni 791 katika idara ya huduma kwa vijana NYS. Katika barua iliyoandikiwa Mkurugenzi wa Upelelezi Ndegwa Muhoro saba hao ambao ni Peter Munyiri  Afisa Mkuu Mtendaji,   Robert Oscar Nyaga, meneja mkuu wa tawi, Charles Kamau Thiongo anayezuia pesa  zisizo halali benki , Raphael Mutinda Nduda-  msimamizi anayezuia hatari kwenye benki, Nancy Njambi -  msimamizi, Meldon Awino Onyango meneja wa mahusiano na josephine Njeri Wairi -  msimamizi wa huduma kwa wateja. Saba hao watafunguliwa mashtaka kwa kosa la kusaidia katika ufujaji wa fedha . Benki kuu ya kenya awali ililazimisha kuachishwa kazi kwa maafisa wakuu 7 wa benki hiyo kuhusiana  na pesa zilizopeanwa kwa josephine kabura. Tobiko ametoa agizo la benki zingine 28 kufanyiwa uchunguzi kuhusiana na sakati hiyo ya nys na ripoti kut