Thomas Bach: wanariadha wa Kenya na Urusi watafanyiwa vipimo dhabiti vya utumizi wa dawa zilizopigw

Sports | Wednesday 22 Jun 2016 7:56 pm
Rais wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki Thomas Bach amesema kuwa wanariadha wa Kenya na Urusi watakaoshiriki mashindano ya Olimpiki watafanyiwa vipimo dhabiti vya utumizi wa dawa zilizopigwa marufuku kabla ya mashindano hayo kuanza. Nchi hizo mbili zimekuwa katika darubini ya I.O.C tangu shirika la kupiga vita dawa hizo (WADA) kusema kuwa hazijatilia maanani kampeni dhidi ya janga hilo. Bach alikuwa akizungumza katika warsha maalum ya kupambana na dawa zilizopigwa marufuku iliyofanyika Brazil. Aidha Bach ameongeza kuwa wanariadha wa Urusi ambao majina yao yatapitishwa na (IAAF) wataruhusiwa kushiriki chini ya mwavuli wa Urusi.