Madaktari wazidi kumuomboleza mwenzao, wanashinikiza vitendea kazi vifaavyo
09, Dec 2020
Madaktari wachanga wamefanya mkutano wa kumkumbuka mwenzao aliyefariki kutokana na virusi vya korona daktari Stephen Mogusu. Madaktari hao hata hivyo wameililia serikali kuangazia maslahi yao na haswa kuwapa vitendea kazi vya kujikinga na maambukizi ya virusi vya korona.