Uhisani wa Standard : Kampuni ya Standard Group yawasaidia wasiojiweza mitaani

KTN News May 22,2020


View More on Dira ya Wiki

Kampuni ya standard group kwa ushirikiano na kampuni ya bima ya GA Insurance, Premier foods, na benki ya I &M wametoa msaada wa chakula kwa zaidi ya familia mia sita, eneo la majengo hapa jijini Nairobi. Kampeni ya ‘Stand with Kenya’ imekuwa ikiendeshwa na kampuni ya standard group ili kuwasaidia wakenya walioathirika kiuchumi na janga la covid 19. Kwa sasa familia zaidi ya elfu tatu zinafaidika na  kampeni hii, ambapo wanaweza kupata chakula cha msaada kila wiki huku wahisani  wakitakiwa kujitokeza kuwasaidia wasiojiweza kipindi hiki kigumu