Wakazi wa sehemu kadha jijini Nairobi wahofia maambukizi ya magonjwa kutokana na uhaba wa maji

KTN News May 21,2020


View More on KTN Leo

Kwa muda sasa wakazi wa kaunti ya Nairobi wamekumbwa na uhaba wa maji baada ya mabwawa yanayoleta maji mjini kuporomoka.

Hata hivyo, hali hiyo ya ukosefu wa maji inatarajiwa kuzorota zaidi, baada ya muungano wa wasambazaji wa maji nchini kusema hakuna hela ya kusambaza maji zaidi.