Watanzania wajiandaa kwa tafrija siku ya jumapili, kusherehekea kupungua kwa maambukizi ya Korona

KTN News May 21,2020


View More on KTN Leo

Wakazi wa jiji la Dar es Salaam nchini Tanzania, wanajiandaa kwa sherehe ya kupungua kwa maambukizi ya virusi vya Korona siku ya Jumapili ya wiki hii kama ilivyotangazwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Hata hivyo sherehe hiyo inaandaliwa wakati ambao hakuna takwimu mpya za mwenendo wa ugonjwa wa Korona kwa wiki ya pili sasa.