.
14th May, 2020
Kufunguliwa kwa shule baada ya kufungwa kwa ajili ya janga la Korona, kutategemea mapendekezo ya kamati maaalum iliyobuniwa na Waziri wa Elimu, Profesa George Magoha, kuangazia athari za Korona kwenye sekta ya Elimu.
Kamati hiyo inawahusisha wanachama tisa wakiwa chini ya uenyekiti wa mwenyekiti wa taasisi ya kutunga na kukuza mitaala nchini, DKT Sarah Ruto.
Hata hivyo chama cha kutetea maslahi ya walimu nchini, KNUT, kimezua maswali baada ya miungano ya walimu kupuuzwa kwenye mchakato mzima.