Walimu 3 wauawa kwa kupigwa risasi katika shambulizi Garissa

KTN News Jan 13,2020


View More on KTN Leo

Siku chache baada ya wanafunzi kuuawa huko Saretho kufuatia shambulizi la Al shabaab, walimu watatu wameuawa usiku wa kuamkia leo katika kijiji cha kamuthey kaunti ya Garissa  Akithibitisha kisa hicho mratibu wa usalama Kaskazini Mashariki Nicodemus Ndalana amesema juhudi za kuwatafuta wanamgambo hao zinaendelea. Hamza yussuf amerejea kutoka kamuthey Garissa.