Gavana wa West Pokot Lonyangapuo akaidi kulipa deni la wizara ya afya

KTN News Dec 13,2019


View More on Leo Mashinani

<style type="text/css">p.p1 {margin: 0.0px 0.0px 0.0px 0.0px; line-height: 20.1px; font: 15.0px 'Microsoft Sans Serif'} span.Apple-tab-span {white-space:pre} </style>

Gavana wa West Pokot Prof. John Lonyangapuo ameiambia wizara ya fedha hatalipa mabaki ya deni kwa wizara hiyo kwani miradi ya uongozi uliopita ilikumbwa na ufisadi wa kupindukia lonyangapuo amesema baadhi ya miradi haikukamilika na kwamba nyingi ilikuwa imehusishwa na ufisadi Lonyangapuo alikuwa akizungumza hapo jana katika hafla ya sherehe za jamhuri katika uwanja wa amakutano kaunti ya West Pokot. West Pokot hata hivyo ilitajwa na wizara ya fedha kama mojawapo ya kaunti ambazo zinadaiwa na wizara hiyo. Lonyangapuo anamtaka waziri Ukur Yattani wa fedha kuomba msamaha kwa kuwapotosha wananchi.