Watu 35 waokolewa kutoka kwa jumba lililoporomoka Tassia

KTN News Dec 08,2019


View More on KTN Leo

Idadi ya watu waliopoteza maisha yao katika jengo lililoporomoka mtaani tassia jijini nairobi imefika saba. Hii ni baada ya watu wawili waliookolewa kutoka vifusi vya jengo hilo usiku wa kuamkia leo kufariki dunia wakipokea matibabu katika hospitali ya kitaifa ya Kenyatta. Shughuli ya uokoaji bado inaendelea huku ikihofiwa kuwa watu 22 bado wamenaswa.