Nordin Haji aamrisha kukamatwa kwa gavana wa Nairobi, Mike Sonko kwa madai ya ufisadi

KTN News Dec 06,2019


View More on Leo Mashinani

Mkurugenzi wa mashtaka ya umma Nordin Haji ameamrisha kukamatwa kwa gavana wa Nairobi Mike Sonko kwa madai ya ufisadi. Nordin akihutubia waandishi wa habari amedai kuwa gavana Sonko atahojiwa kuhusiana na kupotea kwa takriban shilingi milioni mia tatu hamsini na saba (357) fedha za kaunti. Haya yanajiri majuma machache baada ya gavana huyo kushindwa kudhibiti tume ya kukabiliana na ufisadi nchini EACC dhidi ya kuchunguza madai ya ufisadi dhidi yake. Haji aidha amesema Sonko atachunguzwa kwa tuhuma za kujipa mali kinyume cha sheria na vile vile ulanguzi wa pesa na hata madai ya uhalifu ambayo yamewahi kumkabili.