Mahakama ya michezo yafutilia mbali uchaguzi wa FKF uliyoandaliwa wiki jana

KTN News Dec 03,2019


View More on Sports

Mahakama ya kutatua mizozo ya michezo imefutilia mbali uchaguzi wa kitaifa wa shirikisho la soka nchini FKF na kubatili matokeo ya chaguzi za mashinani zilizofanyika mwezi jana. Kufuatia rufaa iliyowasilishwa na kundi linaloongozwa na aliyekuwa mwenyekiti wa FKF Sam Nyamweya,rais wa mahakama hiyo John Ohaga katika uamuzi wake ametilia shaka bodi ya uchaguzi ya shirikisho hilo, akiitaka FKF kuunda bodi mpya. Hata hivyo Ohaga amesisitiza kwamba rais wa shirikisho la soka nchini Nick Mwendwa na uongozi mzima utasalia ofisini kushughulikia  utaratibu wa uchaguzi mpya.