Kundi la inua mama yashtumu vikali tukio la jumanne ambapo mtu mmoja aliwarushia Gesi ya machozi

KTN News Dec 03,2019


View More on KTN Leo

Wabunge ishirini kutoka kundi la ‘inua mama’ wameshutumu vikali kisa cha siku ya ijumaa ambapo mtu mmoja alirusha kitoa machozi kwenye mkutano wa hadhara waliokuwa wameandaa mjini Wajir na kukitaja kama kitendo cha kigaidi. wakiongozwa na mbunge wa kaunti ya Kirinyaga, Wangui Ngirichi, wabunge hao wametaka idara ya polisi kufanya uchunguzi wa haraka na kuwafungulia mashtaka waliohusika kwenye njama hiyo.  Maafisa wa polisi walimkamata, Ali Yasin Mohamed, mkazi wa kibra, ambaye anasaidia kwenye uchunguzi.