Msichana mmoja afariki baada ya kusombwa na maji Rongai kaunti ya Kajiado

KTN News Dec 03,2019


View More on KTN Leo

Msichana mwenye umri wa miaka ishirini, amekufa maji asubuhi ya leo katika mto Kandisi eneo la Olekasasi kule Ongata Rongai. Kulingana na familia ya mzee Mutuku, msichana huyo Anna Nduku alijaribu kumuokoa mwanamume aliyekuwa akijaribu kuvuka mto huo kutoka Rongai na katika pilka pilka   hiyo akateleza na kusombwa na maji.