Serikali ya kaunti ya Meru yazindua mashindano ya Afrika ya mbio za milimani | Zilizala Viwanjani
03, Dec 2019
Serikali ya kaunti ya Meru imezindua mashindano ya Afrika ya mbio za milimani ili kuchangisha fedha za kukabiliana dhidi ya saratani. Mashindano hayo aidha yatatumika kuboresha mazingira na kuvutia watalii. Mbio hizo zitafanyika taerehe 22 Februari mwaka 2020 huku zaidi ya wanariadha elfu 5 wakitarajiwa kushiriki.