Standard kushirikiana na Daystar, kufadhili vipindi vya Transform Kenya

KTN News Nov 29,2019


View More on Dira ya Wiki

<style type="text/css">p.p1 {margin: 0.0px 0.0px 0.0px 0.0px; line-height: 20.1px; font: 15.0px 'Microsoft Sans Serif'} </style>

Shirika La Habari La Standard Limetia Saini Mkataba Na Chuo Kikuu Cha Daystar Kufadhili Msururu Wa Vipindi Vya Transform Kenya Vilevile Kipindi Cha Dau La Elimu Ambacho Hupeperushwa Katika Runinga Ya Ktn News. Akizungumza Wakati Wa Hafla Ya Kusaini Mkataba Huo Katika Ofisi Kuu Ya Standard Group Kwenye Barabara Kuu Ya Mombasa, Naibu Mkuu Wa Chuo Cha Daystar, Prof. Laban Ayiro Ameelezea Matumaini Kwamba Ushirikiano Huo Utafanikisha Na Hasa Kuboresha Sekta Ya Elimu Na Kiswahili Kupitia Kipindi Cha Dau La Elimu Kwa Kutoa Usaidizi Wa Wataalam Wa Kujadili Mada Mbalimbali. Kwa Upande Wake Mkurugenzi Wa Mauzo Katika Standard Group, Irene Kimani Amesema Anatarajia Ufanisi Zaidi Wa Misururu Ya Vipindi Vya Transform Kenya Katika Ushirikiano Na Daystar Ambayo Itachangia Pakubwa Katika Maandalizi Ya Vipindi Vyenyewe Ambavyo Vimekuwa Vikihusisha Mada Kadhaa Zikiwamo Elimu, Uongozi, Kilimo, Afya Na Kadhalika.