16th March, 2019
Gwiji wa raga nchini Collins Injera aliifungia timu ya raga ya Mwamba alama 15 na kuisaidia kupata ushindi wa alama 46?19 dhidi ya timu ya homeboyz kwenye raundi ya 13 ya mashindano ya raga ya kenya cup iliyochezwa ugani impala siku ya jumamosi .katika mechi nyengine ambazo zilichezwa hii leo, nakuru imeilaza impala alama 20?15,kcb wakapata ushindi wa alama 50?5 dhidi ya nondies, nao kenya harlequins wakatoka sare ya alama 22?22 na menengai oilers.