.
5th March, 2019
Usimamizi wa chuo anwai cha Kitale umeifunga taasisi hio kutokana na mgomo wa wanafunzi uliozua rabsha. Kwa siku ya pili mfululizo, wanafunzi hao walisababisha ghasia ndani ya taasisi hio wakilalamikia nyongeza ya ada ya mitihani wakimlaumu msimamizi mkuu fanuel onyango kwa kuwaonea. Wanafunzi hao walimlaumu msimamizi mkuu kwa kuongeza ada hizo na wengine kurejelea mitihani bila kuwafahamisha. Tangu jana, wanafunzi 24 wamekamatwa na maafisa wa polisi kwa kuzuia na kuyarushia mawe magari katika barabara kuu ya kitale ? kipsongo. Hata hivyo, mwalimu mkuu Onyango alidinda kuzungumza na wanahabari waliotaka kusikia upande wake.