Gavana wa Benki kuu ya Kenya, Patrick Njoroge afika mbele ya kamati ya Bunge kuhusu fedha

KTN News Feb 26,2019


View More on KTN Leo

Gavana wa Benki kuu ya Kenya, Patrick Gjoroge, leo hii amefika mbele ya kamati ya Bunge kuhusu fedha na kutetea kanuni alizozichapisha hivi majuzi kuhusu kiwango cha juu cha fedha mtu anastahili kutoa kutoka kwa akaunti. Ingawa Gavana Njoroge alifafanua kwamba hatua hiyo inalenga kuimarisha usalama wa fedha, wabunge walimkashifu kwa kuunda sheria na kanuni bila kuhusisha bunge. Miongoni mwa mapendekezo kwenye sheria hizo mpya alizochapisha gavana wa cbk, ni kwamba wateja wa benki hawataruhusiwa kutoa zaidi ya shilingi milioni moja kwa siku kutoka akaunti zao.