Wakazi wa eneo la mpaka wa Trans Mara na Kisii wameletwa pamoja kuzika tofauti zao

KTN News Feb 19,2019


View More on KTN Leo

Wakazi wa eneo la mpaka wa Trans Mara na Kisii sasa wameletwa pamoja ili kuzika tofauti zao kupitia mpango wa kilimo cha pamoja cha chai kwenye ardhi ekari mia tatu hamsini. Eneo hilo limekuwa sugu kwa uhasama baina ya jamii hizo mbili, kutokana n awizi wa mifugo, lakini sasa kupitia serikali kuu ikishirikiana na  mamlaka ya maendeleo ya ewaso nyiro, uhasama huo unapata suluhu.