Mwamume wa miaka 23 amekamatwa baada ya kudaiwa kumbaka mama

KTN News Feb 18,2019


View More on KTN Leo

Mwamume wa miaka 23 amekamatwa eneo la mui kaunti ya kitui baada ya kudaiwa kumbaka mama aliye na mtoto wa miezi miwili. Mwangangi sammy anadaiwa kumvamia mama huyo nyumbani kwake eneo la mui, akamuwekea vitambaa mdomoni mwake ili Asipige mayowe, na kisha akambaka.mumewe mwathirwa moses musyoka anadai kuwa mhusika wa kitendo hicho ambaye ni jamaa yao alitekeleza kitendo hicho mwendo wa saa nne usiku.akithibitisha kisa hicho, ocpd wa mwingi paul munene amesema mshukiwa ambaye bado anazuiliwa na polisi atafikishwa mahakamani hapo kesho.