Shirikisho la Magongo kuweka madaraja ya mashindano ya vijana

KTN News Feb 16,2019


View More on Sports

Shirikisho la magongo nchini limezindua mradi wa magongo unaopania kukuza na kuendeleza talanta kwenye mchezo huo afrika mashariki.mradi huo wa wachezaji watano kila upande unalenga kuwa kama daraja la kuwawezesha wachezaji wachanga kushiriki mashindano ya wachezaji waliokomaa kitaifa na hata kimataifa.kenya ilikuwa moja kati ya timu za kwanza kuliwakilisha bara la afrika kwenye mashindano ya vijana ya olympiki nchini argentina ambapo timu ya wachezaji watano kila upande kutoka afrika ilishirikishwa.