Familia mjini Nakuru itazika mwili wa baba yao baada ya hospitali kusalimu amri

KTN News Feb 11,2019


View More on KTN Leo

Hatimaye familia moja mjini Nakuru imepata fursa ya kuzika mwili wa baba yao aliyefariki miezi nane iliyopita. Hii imewezekana baada ya hospitali ya Nakuru war memorial kusalimu amri na kuachilia mwili wa marehemu elvis mwaura. Mwili huo ulikuwa umezuiliwa  baada ya familia ya marehemu kushindwa kulipa deni la shilingi milioni mbili na nusu ambayo ni gharama ya matibabu na ada ya kuhifadhia maiti.